NILICHOJIFUNZA SAFARINI: MAWAKALA WA MABASI HUWAPANDISHIA NAULI ABIRIA!

Kila kituo cha Mabasi kina Mawakala wa Mabasi ambao ndio wanaotoa tiketi za safari na kutafuta abiria, hawa ndio walioitwa WAPIGADEBE siku za nyuma.
Hoja hapa ni kuwa abiria anapofika hudakwa na Mawakala na kuelekezwa basi liendalo aendako lakini nauli huambiwa tofauti na ile HALISI hasa kama ni mgeni katika njia hiyo.
Mahali pa 3,000/= huambiwa 5,000/=, pa 6,000/= utasikia 8,000/= nk yote hayo yakiwa ni jitihada ya Mawakala kutengeneza ziada ambayo wao hujilipa kama sehemu ya ASILIMIA ya mauzo ya tiketi inayotokana na juhudi binafsi ya KUMWAMINISHA abiria kuwa hiyo ndiyo nauli halali. Kwa njia hii abiria wanapandishiwa nauli.
NI VEMA SASA, SUMATRA irudishe utaratibu wa karne ya 20, utaratibu wa kubandika MAJEDWALI ya viwango vya nauli kwenye GARI kwa NJIA husika ili ABIRIA aweze kujiridhisha kwa TOZO la Nauli.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s